Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratut Takaathur

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1,2. Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!
Rudi kwenye sura

* 1,2. Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!
Rudi kwenye sura

* 3. Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.
Rudi kwenye sura

* 4. Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!
Rudi kwenye sura

* 5. Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.
Rudi kwenye sura

* 6. Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.
Rudi kwenye sura

* 7. Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.
Rudi kwenye sura

* 8. Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani