| 102.Surat At-Takaathur |
| Imeshuka Makka | Ina aya 8 |
| Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
1

2Mpaka mje makaburini!

3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
3

4. Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
4

5. Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
5

6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
6

7. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
7

8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
8
| Sura Nyingine | Faharasa |