Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Qadr

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.
Rudi kwenye sura

* 2. Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?
Rudi kwenye sura

* 3. Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.
Rudi kwenye sura

* 4. Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.
Rudi kwenye sura

* 5. Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani