| 97.Surat Al-Qadr |
| Imeshuka Makka | Ina aya 5 |
| Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku
wa Cheo Kitukufu.
1

2. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
2

3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
3

4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola
wao Mlezi kwa kila jambo.
4

5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
5
| Sura Nyingine | Faharasa |