1.Suurat al-Faatih'a |
Imeshuka Makka | Ina aya 7 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
1. KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 1
2. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; 2
3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; 3
4. Mwenye kumiliki siku ya malipo. 4
5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. 5
6. Tuongoe njia iliyonyooka. 6
7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. 7
Sura Nyingine | Faharasa |