99.Surat Az-Zilzalah |
Imeshuka Madina | Ina aya 8 |
Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0
1. Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! 1
2. Na itakapo toa ardhi mizigo yake! 2
3. Na mtu akasema: Ina nini? 3
4. Siku hiyo itahadithia khabari zake. 4
5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
6. Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! 6
7. Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! 7
8. Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! 8
Sura Nyingine | Faharasa |