Az Zil-zalah
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratuz zil-zilzalah

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!
Rudi kwenye sura

* 2. Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!
Rudi kwenye sura

* 3. Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?
Rudi kwenye sura

* 4,5. Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua, kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.
Rudi kwenye sura

* 4,5. Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua, kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.
Rudi kwenye sura

* 6. Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura

* 7. Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.
Rudi kwenye sura

* 8. Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani