Lahab maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Utangulizi:
Rudi kwenye sura
* 1. Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.
Rudi kwenye sura
* 2. Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.
Rudi kwenye sura
* 3. Ataingia katika Moto unao waka, aungue.
Rudi kwenye sura
* 4. Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).
Rudi kwenye sura
* 5. Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.
Rudi kwenye sura
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani